WAZIRI AWESO AMSWEKA RUMANDE MHANDISI WA MAJI SHINYANGA, AAGIZA WAHANDISI KUTEMBELEA MIRADI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI AWESO AMSWEKA RUMANDE MHANDISI WA MAJI SHINYANGA, AAGIZA WAHANDISI KUTEMBELEA MIRADI

Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso ameliagiza jeshi la polisi mkoani Shinyanga kumkamata mhandisi wa maji Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Sylivester Mpemba kushindwa kusimamia kikamilifu utekelezaji wa mradi wa maji uliogharimu serikali kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni moja.
Agizo hilo amelitoa  jana Januari 8,2019 wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Mwakitolyo kwenye mkutano wa hadhara ambapo wananchi waliopewa nafasi ya kuuliza maswali walijikita na changamoto ya upatikanaji wa maji kutokana na mradi uliopo kushindwa kutoa maji. Hata hivyo majibu ya mhandisi wa maji Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Sylivester Mpemba yalishindwa kujitosheleza licha ya serikali kutoa fedha kiasi cha shilingi bilioni moja,milioni mia nne na sitini na mbili. 
Kufuatia kukosekana kwa majibu kuhusu namna pesa hizo zilivyotumika,Aweso alieleza kusikitishwa na ucheleweshwaji wa mradi huo akidai kuna uzembe wa Mhandisi huo hivyo kumwagiza Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko na jeshi la polis... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More