Waziri Jafo kufungua mkutano mkuu wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Waziri Jafo kufungua mkutano mkuu wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri


Charles James, Michuzi TV
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mh Suleiman Jafo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano mkuu wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri utakaofanyika jijini Dodoma kuanzia Agosti 20 hadi 24 Mwaka huu.
Akizungumzia mkutano huo Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe wa TAMISEMI, Dk Ntuli Kapologwe amesema kauli mbiu ya mkutano huo itakua ni uajibikaji ni nguzo muhimu katika utoaji huduma bora za afya kuelekea uchumi wa kati.
Amesema mkutano wa mwaka huu utakua ni tofauti na mikutano mingine kutokana na kuanzisha ushirikiano wa karibu baina yao na Wizara ya Afya huku pia wakiwakaribisha Wakurugenzi wa Hospitali mbalimbali ikiwemo Hospitali ya Taifa Muhimbili, Hospitali Maalum ya Jakaya Mrisho Kikwete, Wakurugenzi wa Hospitali za Kanda na wadau wengine.
" Ukiachia hao pia tutakua na Makatibu wa Afya wa Mikoa na moja ya vitu tutakavyofanya katika mkutano huu ni kufanya tathimini ya kipindi cha mwaka mmoja uliopita kuhusiana na utekelezaji wa af... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More