WAZIRI KAIRUKI AAGIZA RITA KUVUNJA BODI YA UONGOZI WA MFUKO WA UDHAMINI WA NORTH MARA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI KAIRUKI AAGIZA RITA KUVUNJA BODI YA UONGOZI WA MFUKO WA UDHAMINI WA NORTH MARA

Na Asteria Muhozya, MaraWaziri wa Madini Angellah Kairuki ameuagiza Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kuvunja uongozi wa Mfuko wa Udhamini wa North Mara ( Bodi ya Wadhamini na Menejimenti) kwa kuwa umeshindwa  kusimamia  uendeshaji wa Mfuko kwa tija na kuandaa utaratibu mzuri  wa usimamizi  wa Mfuko huo ambao utakuwa na  manufaa kwa Taifa .
Aidha, Waziri Kairuki amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Tarime kuruhusu fedha za Keng'anya Enterprises Ltd ( KEL) kuendelea kulipwa  hadi hapo vyombo vya uchunguzi vitakakapobaini na kuelekeza vinginevyo, huku Mkuu wa Mkoa wa Mara akitakiwa kusimamia utekelezaji wa agizo hilo.
“Kwa kuwa Keng'anya Enterprises iliomba kupata PL 303/95 kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia Sekta ya Madini, hivyo malipo ya mrabaha wa asilimia moja yanayopokelewa kutoka kwenye mgodi kwa mujibu wa mkataba wake ni halali,” alisisitiza Kairuki.
Waziri Kairuki  alitoa  maagizo hayo Novemba 21, ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri y... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More