WAZIRI KAIRUKI NA UBALOZI WA KUWAIT WAWAFARIJI WAHANGA WA MAFURIKO SAME. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI KAIRUKI NA UBALOZI WA KUWAIT WAWAFARIJI WAHANGA WA MAFURIKO SAME.

Na Dixon Busagaga,Same.
UBALOZI wa Kuwait nchini Tanzania umetoa jumla ya tani saba za msaada wa Chakula kwa waathirika wa Mafuriko wilayani Same mkoani Kilimanjaro ambao walilazimika kuyahama makazi yao katika Vijiji vya Kajiungeni na Ruvu Marwa na kuhamishiwa katika Makambi.
Msaada huo uliowasilishwa na Baloziw wa Kuwait nchini ,Jaseen Al Najem umetokana na jitihada za Waziri wa Madini ,Angela Kairuki za kusaidia kaya zilizofikwa na athari ya mafuriko hayo ambapo yeye binafsi alitoa Blanketi 300 na Turubai 200 kwa ajili ya wathirika hao kujisitiri.
Akizungumza wakati wa kukabidhi Msaada huo ,Balozi wa Kuwait ,Al Najeem amesema mbali na msaada huo anatarajia kuzungumza na Shirika la Huduma ya kwanza la nchini Kuwait kuona namna ambavyo watashirikiana na Shiriki la Msalaba mwekundu kusaidia wananchi hao.
Akitoa taarifa ya athari ya Mafuriko hayo Mkuu wa wilaya ya Same ,Rosemery Senyamule amesema wananchi wamekubalina kuhama kutoka eneo la Mafuriko ambalo wamekuwa wakifanya shughuli za Kilimo na kupewa maeneo ambayo sasa watafanya makazi ya kudumu.Balozi wa Kuwait nchini Tanzania ,Jaseen Al Najem akikabidhi msaada wa Chakula kwa wananchi wa eneo la Kombo wilayani Same.kushoto ni Waziri wa Madini,Angela Kairuki na Mkuu wa wilaya ya Same,Rosemery Senyamule.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza Waziri wa Madini ,Angela Kairuki aliyeongozana na Balozi wa Kuwait nchini ,Jaseen Al Najem kutoa msaada kwa Wahanga hao.

Waziri wa Madini,Angela Kairuki akikabidhi msaada wa Blanketi na Maturubai kwa ajili ya kujengengea mahema ya muda kwa wahanga wa Mafuriko katika wilaya ya Same.Waziri wa Madini,Angela Kairuki akisalimiana na mmoja wa Wazee ambao kwa sasa wanahifadhiwa na Majirani baada ya nyumba yake kuzingirwa na Mafuriko .

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Source: Issa MichuziRead More