WAZIRI KALEMANI AWASIMAMISHA KAZI WATENDAJI TANESCO KWA KUSHINDWA KUWASHA UMEME VIJIJINI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI KALEMANI AWASIMAMISHA KAZI WATENDAJI TANESCO KWA KUSHINDWA KUWASHA UMEME VIJIJINI

Na Leandra Gabriel, blogu ya jamii
WAZIRI wa Nishati Dkt.Medard Kalemani amefanya ziara katika Wilaya ya Mkuranga katika kukagua utekelezaji wa utoaji wa huduma ya umeme kwa wananchi na hakuridhishwa na utendaji wa baadhi ya wahusika katika idara hizo na kuamua kuwaweka kando ili wenye kasi watekeleze jukumu hilo.
Katika Ziara hiyo Kalemani  amemuagiza meneja Tanesco  mkoa wa Pwani kumsimamisha kazi  Mhandisi wa Mkoa na  pia amemuagiza meneja wa wilaya ya Mkuranga Mhandisi, Regina Mvungi kumsimamisha mhandisi mwenye dhamana hiyo katika wilaya ya Mkuranga kwa kushindwa kufanya kazi ya kuwasha umeme kwenye vijiji vilivyo kwenye mradi kata ya Vikundi.
Aidha Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani ametoa siku 14 Wilayani Mkuranga katika  kuhakikisha umeme unawaka katika vijiji vyote vilivyokatika mpango huo.Waziri hiyo aliyasema hayo Leo hii wakati wa ziara ya kutembelea wilayani Mkuranga ili kuona namna ya upatikanaji wa huduma ya Nishati ya Umeme katika Kata ya Kisiju,Vikin... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More