WAZIRI KALEMANI KUTOA MUELEKEO WA NCHI KATIKA KUTUMIA NISHATI YA MAFUTA NA GESI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI KALEMANI KUTOA MUELEKEO WA NCHI KATIKA KUTUMIA NISHATI YA MAFUTA NA GESI

*Ni kupitia Kongamano la pili la sekta ya mafuta, gesi litalokafanyika Septemba 24/25
Na Said Mwishehe, Globu ya jamiiSERIKALI kupitia Waziri wa Nishati Dk.Medard Kalemani inatarajia kuzungumzia mwelekeo wa nchi katika kutumia nishati ya mafuta na gesi katika viwanda.
Waziri Kalemani atatoa muelekeo huo katika Kongamano la Pili la Sekta ya Mafuta na Gesi linalotarajia kufanyika kuanzia Septemba 24 hadi 25 mwaka huu jijini Dar es Salaam.Mbali ya Waziri kutoa mwelekeo, pia wadau muhimu wa sekta ya mafuta na gesi wakiwamo TPDC, PURA,EWURA, NEEC, ATOGS na TPSF watashiriki.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam kuhusu kongamano hilo Abdulsamad Abdulrahim kutoka Shirikisho la Watoa Huduma za Mafuta na Gesi nchini amesema Serikali na wadau wa sekta ya mafuta na gesi wameunga mkono na watashiriki kikamilifu.
Amefafanua kongamano hilo limeandaliwa na Pietro Fiorentini Tanzania kwa kushirikiana na CWC Group ambapo pamoja na mambo mengine mradi wa bomba la mafuta ghafi utachambuliwa wakati wa kongamano... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More