WAZIRI KAMWELWE ATAKA KASI UJENZI WA BARABARA MKOANI RUVUMA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI KAMWELWE ATAKA KASI UJENZI WA BARABARA MKOANI RUVUMA

IMEELEZWA kuwa kukamilika mapema kwa barabara za lami na madaraja ya kisasa katika mkoa wa Ruvuma kutauunganisha kirahisi na mikoa ya nyanda za juu kusini na nchi za jirani na hivyo kuhuisha uchumi wa wakazi wake.Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe amesema hayo alipokagua ujenzi wa barabara ya Mbinga-Mbamba Bay KM 60 na kumtaka mkandarasi china Henan International Cooperation Group Co. Ltd (CHICO), anayejenga barabara hiyo kuikamilisha kwa wakati.Amesema fursa za kilimo, uvuvi, usafirishaji na uchukuzi wa mazao na makaa ya mawe katika mkoa wa Ruvuma zinahitaji barabara za lami na zenye uwezo wa kupitika wakati wote na kwa urahisi hivyo kukamilika kwa barabara za lami kwa wakati kutaleta ukombozi kwa wananchi wa mkoa huo.“Viwanda vingi sasa vinatumia makaa ya mawe tena kwa kiwango kikubwa hivyo tunahakikisha usafiri katika mkoa huu unakuwa wa uhakika ili kuufungua na kuunganisha na mikoa mingine kwa njia fupi  na  hivyo kuongeza biashara ya ndani k... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More