WAZIRI KAMWELWE KUFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA WADAU WA BARABARA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI KAMWELWE KUFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA WADAU WA BARABARA

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, anatarajiwa kufungua mkutano wa kimataifa kuhusu mapinduzi ya sekta ya usafirishaji na mabadiliko ya kiuchumi katika nchi zinazoendelea, jijini Arusha. 
Mkutano huo wa siku mbili (2) ulioandaliwa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa kushirikiana na Shirikisho la Barabara Duniani (World Road Association-PIARC), utafanyika katika ukumbi wa kimataifa wa AICC. 
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Sekta ya Ujenzi, Mhandisi Joseph Nyamhanga, amesema maandalizi kwa ajili ya mkutano huo yamekamilika ambapo takribani washiriki zaidi ya 200 kutoka nchi 25 duniani watashiriki mkutano huo. 
Mkutano huo ambao lengo lake kuu ni kuangalia matokeo ya uwekekezaji katika mundombinu ya usafirishaji utajadili kwa kina mada mbalimbali zinazohusu changamoto zinazozikabili nchi zinazoendelea ikiwemo rasilimali chache za kuimarisha miundimbinu ya usafirishaji wakati huohuo kuboresha huduma nyingine za kijamii kama vile maji, afya, elimu na... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More