WAZIRI KANGI LUGOLA AAGIZA WANAOSAMBAZA PICHA ZA WATU WALIOFARIKI KWENYE AJALI YA KIVUKO WASHUGHULIKIWE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI KANGI LUGOLA AAGIZA WANAOSAMBAZA PICHA ZA WATU WALIOFARIKI KWENYE AJALI YA KIVUKO WASHUGHULIKIWE

 Waziri wa Mambo ya Ndani mheshimiwa Kangi Lugola ameagiza kuchukuliwa hatua za kisheria kwa watu wanaosambaza picha za watu waliopoteza maisha kwenye ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea juzi Septemba 20,2018.

Waziri Lugola ameviagiza vyombo vinavyohusika kufuatilia wanaosambaza picha hizo kwa ni kinyume cha sheria za makosa ya mtandao.

Tangu jana kumezuka tabia kwa baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii ikiwemo whatsapp,instagram na facebook wamekuwa wakisambaza picha za watu waliofariki kwenye ajali ya kivuko cha MV Nyerere kwenye magroup na wengine kupost kwenye kurasa zao kitendo ambacho ni kinyume cha sheria,utu na maadili.... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More