WAZIRI LUGOLA AANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI ARUSHA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI LUGOLA AANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI ARUSHA
 
WAZIRI wa Mambo ya ndani ya Nchi,Kangi Lugola Na. Vero Ignatus, Arusha

WAZIRI wa Mambo ya ndani ya Nchi,Kangi Lugola amelitaka Jeshi la Polisi nchini kushirikiana na mamlaka ya ya Mawasiliano nchini TCRA,ili kuweza kuwabaini wale wote wanaovunja Amani ya nchi,kwa kutumia njia ya Mtandao.

Ameyasema hayo Jijini Arusha Wakati akiwa katika ziara yake ya siku nane,lengo likiwa ni kufanya mikutano ya hadhara na kusikiliza maoni ya wananchi juu ya Usalama anaousimamia.Lugola amesema kuwa kwa sasa nchi ina Amani ya Kutosha na hivyo asitokee mtu wa kuvuruga Amani hiyo.

Aidha waziri Lugola ametoa wito kwa watanzania kuendelea kuliamini Jeshi la Polisi ,katika ufanisi wa kazi zao za kulinda raia na mali zake.Amesema mitandao ya kijamii inaweza kutumika kuleta maendeleo badala ya kuchochea Uvunjifu wa Amani.

Waziri Lugola yupo mmkoani Arusha ambapo anatarajiwa kufanya ziara yake ya kikazi ya kutembelea Wilaya zote Saba za Mkoa wa Arusha.... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More