WAZIRI LUGOLA AKUTANA NA WATUMISHI WA WIZARA YAKE, AWATAKA WACHAPE KAZI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI LUGOLA AKUTANA NA WATUMISHI WA WIZARA YAKE, AWATAKA WACHAPE KAZI

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na watumishi wa Wizara yake (hawapo pichani), kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji kazi. Lugola aliwataka watumishi hao kufanya kazi kwa bidii pamoja na changamoto zote zinazowakabili na atashirikiana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu (kushoto), wanatatua changamoto za watumishi hao. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhan Kailima. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha Veta, jijini Dodoma, leo. Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo (mstari wa mbele) wakiwa na watumishi wengine wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakimsikiliza Waziri wa Wizara hiyo, Kangi Lugola (hayupo pichani), wakati alipokua akizungumza na watumishi hao kwa mara ya kwanza tangu alipoteuliwa kuiongoza wizara hiyo. Katika hotuba yake, Lugola aliwataka watumishi hao kufanya kazi kwa bidii, pia aliwahidi watumishi hao atashirikiana na Katibu Mkuu kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili katika utendaji wao... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More