WAZIRI LUGOLA AONYA POLISI KUTUMIWA NA MAFISADI KUPORA ARDHI ZA WANANCHI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI LUGOLA AONYA POLISI KUTUMIWA NA MAFISADI KUPORA ARDHI ZA WANANCHI

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Kijiji cha Ragati, Jimbo la Mwibara, Wilayani ya Bunda, mkoani Mara, jana. Katika hotuba yake, Lugola aliwaonya Polisi nchini ambao wanatumiwa na mafisadi kuwanyanyasa wananchi maskini kwa kupora ardhi zao na kukimbilia kufungua kesi vituoni wakilazimisha ardhi hiyo kuwa ni mali yao.
Na Felix Mwagara, MOHA
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewaonya Polisi nchini ambao wanatumiwa na mafisadi kuwanyanyasa wananchi maskini kwa kupora ardhi zao na kukimbilia kufungua kesi vituoni wakilazimisha ardhi hiyo iwe mali yao.
Akizungumza na mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Ragati, Kata ya Kasuguti, Jimbo la Mwibara, wilayani Bunda, Mkoa wa Mara, Lugola alisema amepata malalamiko mengi kutoka sehemu mbalimbali nchini, kuwa mafisadi uonea wananchi maskini kwa kupora kwa nguvu ardhi wakidai wanamiliki wao na wanatumia b... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More