WAZIRI LUGOLA APIGA MARUFUKU WATUMISHI WIZARA YAKE KUNYANYASWA, AFUNGUA MILANGO KULETA KERO ZAO OFISINI KWAKE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI LUGOLA APIGA MARUFUKU WATUMISHI WIZARA YAKE KUNYANYASWA, AFUNGUA MILANGO KULETA KERO ZAO OFISINI KWAKE

Na Felix Mwagara, MOHAWAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka viongozi na watumishi mbalimbali wa wizara yake wafanye kazi kwa kushirikiana na kuacha tabia ya kunyanyasana wakati wanatekeleza majukumu yao ya kikazi.
Lugola pia amesema kila mtumishi wa wizara yake ana umuhimu mkubwa kwa kufanikisha mafanikio ya wizara hiyo kwakuwa watumishi hao wanafanya kazi kwa kutegemeana. Akizungumza na watumishi wa makao makuu wa wizara hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Veta, jijini Dodoma jana, Lugola alisema kikao hicho alikiitisha kwa lengo la kujuana na watumishi hao pamoja na kujua changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi.
“Mambo muhimu ambayo yatatuletea mafanikio ndani ya wizara yetu ni kufanya kazi kwa bidii, kufanya kazi kwa kushirikiana na tukifanya hivyo hakika tutapendana na kuzidi kufanikiwa,” alisema Lugola.
Lugola aliongeza kuwa, hapendi kuona mtumishi yeyote ananyanyaswa kwa kutopewa haki zake au kucheleweshewa pasipo kuwa na s... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More