WAZIRI LUGOLA AWASIMAMISHA KAZI VIGOGO WATANO SAKATA LA KUNASWA SARE ZA JESHI KAMBI ZA WAKIMBIZI MKOANI KIGOMA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI LUGOLA AWASIMAMISHA KAZI VIGOGO WATANO SAKATA LA KUNASWA SARE ZA JESHI KAMBI ZA WAKIMBIZI MKOANI KIGOMA

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Kangi Lugola   *Aagiza wachunguzwe, atoa maagizo mazito kwa Katibu Mkuu Mambo ya Ndani

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii


WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Kangi Lugola amewasimamisha kazi vigogo watano wanaohusika na wakimbizi katika kambi ya Mtendele na Nduta mkoani Kigoma, baada ya kubainika uwepo wa sare za Jeshi zikiwa kwenye marobota ya nguo za misaada.

Akizungumza leo Januari 13,2019 , Waziri Lugola amesema kumebainika uwepo wa sare hizo kwenye marobota hayo ya nguo za misaada ambazo yalikuwa yanapelekwa katika kambi ya Wakimbizi Mtendeli na Kambi ya wakimbizi ya Nduta mkoani Kigoma.

Amefafanua katika kambi ya Mtendeli kumebainika kuwepo kwa sare za jeshi 1325 na katika kambi ya Nduta kumebainika uwepo wa sare 622 na hivyo kufanya jumla ya idadi ya sare zote kuwa 1947.

"Kwa Serikali hii inayoongozwa na Rais Dk.John Magufuli haiko tayari kuona tukio hilo linaachwa bila kuchukua hatua.Kama nguo hizo zimeweza kubainika maana yake kesho au kesh... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More