WAZIRI MAKAMBA AUNGANA NA WANA KIZIMKAZI KUADHIMISHA SIKU YAO, ACHANGIA MIFUKO 50 YA SARUJI NA BATI 50 - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI MAKAMBA AUNGANA NA WANA KIZIMKAZI KUADHIMISHA SIKU YAO, ACHANGIA MIFUKO 50 YA SARUJI NA BATI 50

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba amehidi kutoa mifuko hamsini ya saruji na bati hamsini kama mchango wake katika ujenzi wa Shule ya awali ya Kizimkazi iliyopo takiriban kilomita 61 kutoka Mjini Unguja. 
Ahadi hiyo ameitoa hii leo Shehia ya Kizimkazi- Mkunguni katika Wilaya ya Kusini, Jimbo la Makunduchi katika maadhimisho ya Siku ya Kizimkazi. “Nawapongeza sana kwa hatua hii mliyofikia na utayari wenu wa kuwekeza katika miradi mikubwa hususan elimu ambayo ndio nguzo kuu” Makamba alisisitiza. 
Waziri Makamba amewataka wana Kizimkazi kuandaa utaratibu wa kutembeleana na kubadilishana uzoefu baina yao na vijiji vya Tanzania Bara ili kudumisha Muungano na kujenga ushirikiano zaidi. “Mwakani tuweke nguvu zaidi, tuwe na vikundi vya ngoma na sanaa mbalimbali kutoka upande wa pili wa Muungano pia tutaanda ziara ya mafunzo ili kwa pamoja muweze kubadilisha uzoefu” alibainisha Makamba. 
Aidha, Waziri Makamba amewakumbusha wana Kizimkazi k... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More