WAZIRI MHAGAMA AMPA MWEZI MMOJA MKANDARASI KUKAMILISHA UJENZI BARABARA YA KUUNGANISHA DARAJA LA NYERERE NA KIGAMBONI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI MHAGAMA AMPA MWEZI MMOJA MKANDARASI KUKAMILISHA UJENZI BARABARA YA KUUNGANISHA DARAJA LA NYERERE NA KIGAMBONI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama amempa mwezi mmoja mkandarasi anayejenga kwa kiwango cha lami barabara yenye urefu wa kilometa mbili inayounganisha Daraja la Nyerere na barabara ya Kibada-Feri iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam, kukamilisha kazi  hiyo hadi tarehe 31 Agosti, mwaka huu, ili kurahisisha mawasiliano kwa wananchi wanaovuka daraja hilo.Waziri Mhagama ameyasema hayo wakati akikagua  ujenzi wa barabara hiyo na kujionea uendeshaji wa shughuli  katika daraja la Nyerere, ambapo amefafanua kuwa kutokamilika kwa ujenzi wa barabara hiyo kunasababisha kero  kwa wananchi wanaovuka kwa miguu na wanaotumia vyombo vya usafiri kushindwa kupita kwa urahisi, hali inayochangia kupungua kwa mapato yanayokusanywa darajani hapo.“Hii barabara ni ya msingi kwani kutokamilika kwake ndo maana hata magari madogo hayapendi kutumia hii njia, Mkandarasi huyu ameomba mara mbili kuongezewa muda kukamilisha ka... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More