WAZIRI MHAGAMA:WAKUU WA MIKOA KANDA YA KASKAZINI TATUENI MIGOGORO YA ARDHI YA WAKULIMA NA WAFUGAJI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI MHAGAMA:WAKUU WA MIKOA KANDA YA KASKAZINI TATUENI MIGOGORO YA ARDHI YA WAKULIMA NA WAFUGAJI

Na.Vero Ignatus Arusha. 
Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu) Jenista Mhagama amewataka Wakuu wa Mikoa ya Kanda ya kaskazini kuhakikisha wanatatua migogoro ya ardhi ya wakulima na wafugaji ili waondokane na tatizo hilo na kujikita kwenye maendeleo. 
Waziri Mhagama ameyasema hayo kwenye maadhimisho ya 25 ya maonyesho ya kilimo na mifugo nane nane kanda ya kaskazini jijini Arusha.Amewataka viongozi hao kutatua migogoro hiyo ili kukuza sekta hizo kwani lengo la serikali ni kuhakikisha matumizi bora ya ardhi yanafanikishwa ili kuongeza tija za kiuchumi. 
Mhe. Jenista amesema kuwa migogoro ya ardhi ya wakulima na wafugaji inachangia kuzorotesha ustawi wa jamii kutokana na migogoro hiyo hivyo viongozi hao wahakikishe wanakomesha tatizo hilo. "Sekta hizo zinatakiwa kuungwa mkono na kuachana na migogoro hiyo ya muda mrefu ambayo haina tija kwa jamii zaidi ya kusababisha mtafaruku na uvunjifu wa amani," alisema. 
Alisema pamoja na kuya... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More