WAZIRI MKUU ABAINI MADUDU FEDHA ZA DAWA MPWAPWA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI MKUU ABAINI MADUDU FEDHA ZA DAWA MPWAPWA

*Amuagiza mkuu wa wilaya afanye uchunguzi kubaini zinapokwenda
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Bw. Jabir Shekimweri afanye uchunguzi kuhusu matumizi ya sh. milioni 70 zinazotelewa kila mwezi na Serikali kwa ajili ya kununulia dawa kwenye wilaya hiyo.
"Kilichokuwa kinasemwa na wabunge bungeni nilidhani sicho, nikasema nakuja niyasikie mwenyewe. Kweli wananchi hawaridhiki nimeona. Sasa mkuu wa wilaya shughulikia hili jambo ili kubaini fedha za dawa zinakwenda wapi.”
Alitoa agizo hilo jana jioni (Jumatano, Oktoba 10, 2018) wakati akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule msingi Mpwapwa, ambapo alipokea malalamiko ya wananchi juu ya ukosefu wa dawa. Dawa pekee wanazopewa ni za kutuliza maumivu tu.
Waziri Mkuu alisema lengo la Serikali kutoa fedha hizo kila mwezi ni kuhakikisha kwamba wananchi wote wanapata huduma za afya popote walipo badala ya kusafiri umbali mrefu kwenda makao makuu ya wilaya.
"Kila mwezi Serikali inatoa ... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More