WAZIRI MKUU AFUNGA TAMASHA LA URITHI FESTIVAL - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI MKUU AFUNGA TAMASHA LA URITHI FESTIVAL

*Atoa miezi miwili Wizara ya Habari ikamilishe mchakato wa vazi la Taifa
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa muda wa miezi miwili na nusu kwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezoiwe imekamilisha mchakato wa Tanzania kuwa na vazi la Taifa.
Amesema Watanzania bado hawajaunganishwa kwa kuwa na vazi la Taifa, ambalo mchakato wake  umeendeshwa kwa miaka mingi na wizara hiyo bila ya kujulikana wamefikia wapi.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Oktoba 13, 2018) wakati akifunga tamasha za Urithi Festival, lililofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini  Arusha.
“Ifikapo Desemba 30,2018 tuwe tumeanza kupata sura ya vazi la Taifa ili wadau walijadili na waamue ni vazi gani la Mtanzania ambalo litawakilisha Taifa kama nchi nyingine walivyomudu kuwa na vazi la Taifa.”
Aliongeza kuwa ili kufikia azma  Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezoiandae tamasha maalumu kwa ajili ya kuonesha aina tofauti za nguo ili kupata vazi la Taifa.
Kadhalika, Waziri Mkuu aliwaagiza wa... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More