WAZIRI MKUU AFUNGUA KIWANJA CHA TAIFA CHA MCHEZO WA BASEBALL - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI MKUU AFUNGUA KIWANJA CHA TAIFA CHA MCHEZO WA BASEBALL

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefungua kiwanja kipya cha Taifa cha mchezo wa Baseball na kuzindua mashindano ya Taifa ya Baseball nchini. Amewaagiza viongozi wa Wizara ya Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni na Ofisi ya Rais-TAMISEMI waone umuhimu wa kuuendeleza mchezo huo.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Desemba 6, 2018) alipofungua kiwanja cha Baseball katika shule ya Sekondari ya Azania, jijini Dar es Salaam. Amesema iwapo mchezo huo utaratibiwa vizuri na kuingizwa katika michezo UMISETA na UMITASHUMTA utaleta tija kwa wanafunzi wanaoucheza nchini.
Waziri Mkuu amesema thamani ya uwanja huo ni takribani Dola za Kimarekani 80.234 ambazo zimetolewa kwa msaada kutoka Serikali ya Japani.Amesema anaishukuru Serikali ya Japan na amefarijika kwa dhamira yao ya kuunga mkono utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi CCM 2015-2020 hususan ibara ya 161.
Waziri Mkuu amesema ilani inaielekeza Serikali kujenga na kuimarisha miundombinu ya michezo nchini na kuifanya sekta ya michezo kutoa ajira hususa... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More