WAZIRI MKUU AHUTUBIA MKUTANO WA HALMASHAURI KUU YA CCT JIJINI DODOMA, AZITAKA TAASISI ZA DINI ZIWEKEZE KWENYE VIWANDA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI MKUU AHUTUBIA MKUTANO WA HALMASHAURI KUU YA CCT JIJINI DODOMA, AZITAKA TAASISI ZA DINI ZIWEKEZE KWENYE VIWANDA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa dini wasibaki nyuma katika suala zima la kuwekeza kwenye viwanda ili waweze kuendana na azma ya Serikali ya awamu ya tano ya kuifikisha Tanzania kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
“Serikali ya awamu ya tano imeazimia kukuza uchumi wa viwanda. Nawaomba msiwe nyuma katika suala hili, tumieni fursa ya ardhi tuliyonayo hasa katika ujenzi wa viwanda vya usindikaji ili kuongeza thamani ya mazao,” amesema. Waziri Mkuu ametoa rai hiyo leo (Alhamisi, Julai 12, 2018) wakati akifungua Mkutano wa Halmashauri Kuu ya 52 ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT). Mkutano huo wa siku mbili, umehudhuriwa na maaskofu zaidi ya 80, wenyeviti wa makanisa na wawakilishi wa vyama vishiriki. Amesema uwepo wa viwanda hivyo utachangia ukuaji wa sekta ya kilimo na kuongeza ukuaji wa mnyonyoro wa thamani ya mazao. Akitoa mfano fursa zilizopo hivi sasa, Waziri Mkuu aliwaeleza Maaskofu hao kwamba bei ya ufuta kwa mwaka huu imepanda na kufikia sh. 3,100/- iki... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More