Waziri Mkuu amaliza sakata la nguzo za umeme lililowahusisha Mawaziri wawili na RC Iringa - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Waziri Mkuu amaliza sakata la nguzo za umeme lililowahusisha Mawaziri wawili na RC Iringa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kampuni zote zinazosambaza nguzo za umeme zinatakiwa zilipe ushuru wa halmashauri wanakotoa nguzo hizo amboa ni asilimia tano ya gharama ya kila nguzo kama ilivyoelekezwa na Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa.

Ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Januari 7, 2019) baada ya kupata taarifa kuhusu kampuni ya New Forest ambayo inamkataba na TANESCO wa kusambaza nguzo za umeme, kwa muda mrefu kampuni hiyo imekuwa ikikaidi kulipa ushuru wa asilimia tano ya gharama ya kila nguzo. Ushuru huo umefikia sh. bilioni 2.9 hali iliyopelekea uongozi wa mkoa kuzuia nguzo hizo zisitoke.

Wiki iliyopita akiwa katika ziara ya mkoa Ruvuma, Waziri Mkuu alipokea malalamiko kuhusu mkoa wa Iringa kuzuia kusambazwa kwa nguzo za umeme ndipo alipoamua kuwaita Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi pamoja na wakuu wa wilaya, wakurugenzi pamoja na wenyeviti wa halmashauri wanaotoka katika wilaya zinazozalisha nguzo.

Viongozi wengine waliohudhuria kikao hicho ni Waziri wa Nchi Of... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More