WAZIRI MKUU AMEMPONGEZA BONDIA HASSAN MWAKINYO, KILIMANJARO QUEENS NA SERENGETI BOYS KWA KUFANYA MAAJABU - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI MKUU AMEMPONGEZA BONDIA HASSAN MWAKINYO, KILIMANJARO QUEENS NA SERENGETI BOYS KWA KUFANYA MAAJABU


WAZIRI MKUU Mhe. Kassim Majaliwa amempongeza mwanamasumbwi wa Kitanzania Hassan Mwakinyo (23) kwa kumchapa bondia Mwingereza Bw. Sam Eggintonkwenye raundi ya pili ya pambano lao la masumbwi lililofanyika Jumapili, Septemba 9, 2018, huko Birmingham nchini Uingereza. Waziri Mkuu ametoa pongezi hizo leo (Ijumaa, Septemba 14, 2018) wakati akiahirisha mkutano wa 12 wa Bunge, Bungeni jijini Dodoma. Bunge limeahirishwa hadi Novemba 6, 2018. Amesema bondia huyo amelipa Taifa heshima kubwa kwa kulitangaza kimataifa katika Nyanja ya michezo, hivyo amewataka wanamichezo wengine nchini waige mfano wake.Wakati huo huo, Waziri Mkuu ameipongeza timu ya Taifa ya Wanawake (Kilimanjaro Queens) kwa kutwaa kombe la Afrika Mashariki. Pia ameipongeza timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) kwa kuwa washindi wa tatu kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kwenye mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF). “Hongereni sana wanamichezo wetu na endelezeni moyo huo ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More