WAZIRI MKUU AMEMPONGEZA MWAKINYO KWA KUMCHAPA MUINGEREZA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI MKUU AMEMPONGEZA MWAKINYO KWA KUMCHAPA MUINGEREZA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amempongeza mwanamasumbwi wa Kitanzania Bw. Hassan Mwakinyo (23) kwa kumchapa bkondia Mwingereza Bw. Sam Egginton.

Bw. Mwakinyo alimchapa Bw Egginton kwenye raundi ya pili ya pambano lao la masumbwi lililofanyika Jumapili, Septemba 9, 2018, huko  Birmingham nchini Uingereza.

Waziri Mkuu ametoa pongezi hizo leo (Ijumaa, Septemba 14, 2018) wakati akiahirisha mkutano wa 12 wa Bunge, Bungeni jijini Dodoma. Bunge limeahirishwa hadi Novemba 6, 2018.

Amesema bondia huyo amelipa Taifa heshima kubwa kwa kulitangaza kimataifa katika Nyanja ya michezo, hivyo amewataka wanamichezo wengine nchini waige mfano wake.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu  ameipongeza timu ya Taifa ya Wanawake (Kilimanjaro Queens) kwa kutwaa kombe la Afrika Mashariki. 

Pia ameipongeza timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) kwa kuwa washindi wa tatu kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kwenye mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).  

“Hongereni sana wanamichezo... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More