WAZIRI MKUU AMEMPONGEZA MWAKINYO KWA KUMCHAPA MUINGEREZA - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI MKUU AMEMPONGEZA MWAKINYO KWA KUMCHAPA MUINGEREZA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Bondia Hassan Mwakinyo kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma Septemba 14, 2018. Mwanamasumbwi huyo hivi karibuni alimtwanga kwa TKO, Bondia Sam Egginton wa Uingereza katika pambano lililofanyika Birmingham. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amempongeza mwanamasumbwi wa Kitanzania Bw. Hassan Mwakinyo (23) kwa kumchapa bkondia Mwingereza Bw. Sam Egginton.
Bw. Mwakinyo alimchapa Bw Egginton kwenye raundi ya pili ya pambano lao la masumbwi lililofanyika Jumapili, Septemba 9, 2018, huko Birmingham nchini Uingereza.
Waziri Mkuu ametoa pongezi hizo leo (Ijumaa, Septemba 14, 2018) wakati akiahirisha mkutano wa 12 wa Bunge, Bungeni jijini Dodoma. Bunge limeahirishwa hadi Novemba 6, 2018.
Amesema bondia huyo amelipa Taifa heshima kubwa kwa kulitangaza kimataifa katika Nyanja ya michezo, hivyo amewataka wanamichezo wengine nchini waige mfano wake.
Wakati huo huo, Waziri Mkuu ameipongeza timu ya Taifa ya Wanawake (Kilimanjaro ... Continue reading ->


Source: KajunasonRead More