WAZIRI MKUU AMUAGIZA SIMBAKALIA AFUATILIE KIBALI WIZARA YA ARDHI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI MKUU AMUAGIZA SIMBAKALIA AFUATILIE KIBALI WIZARA YA ARDHI


*Ni cha ujenzi wa kiwanda cha nyuzi Chalinze
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa EPZA, George Simbakalia afuatilie Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuhusu kibali cha ujenzi wa kiwanda cha nyuzi kinachotakiwa kujengwa Chalinze. Ametoa agizo baada ya Mkuu wa mkoa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo kumuleza kuwa kuna muwekezaji wa kiwanda cha kutengeneza nyuzi cha H and J cha Chalinze ambacho ujenzi wake umekwama kutokana na mwekezaji kutopewa kibali cha ardhi.
Waziri Mkuu ametoa agzo hilo leo (Ijumaa, Desemba 7, 2018) alipozungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha Keda kinachotengeneza marumaru aina ya Twyford kilichopo Chalinze mkoani Pwani akiwa njiani kwenda jijini Dodoma.
Waziri Mkuu amesema ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imedhamiria kuwaunga mkono wawekezaji na kuwafanya wawekeze bila ya urasimu, hivyo amemuagiza kiongozi huyo wa EPZA kuhakikisha kibali kinapatikana.“Nakuagiza Mkurugenzi ufuatilie kibali hicho na nikifika Dodoma... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More