Waziri Mkuu anataka taji la AFCON U17 libaki nyumbani - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Waziri Mkuu anataka taji la AFCON U17 libaki nyumbani

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameliangiza hirikisho la soka nchini TFF lihakikishe Tanzania inaibuka na ushindi katika fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 mwaka 2019.


Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo asubuhi February 7, 2019 Bungeni jijini Dodoma katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu wakati akijibu swali la Mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto ambaye alitaka kufahamu, serikali inayahusishaje mashindano hayo ya AFCON na mkakati wa kuendeleza utalii nchini.


Waziri Mkuu amesema maandalizi yote yanaendelea kufanyika na serikali imejiandaa vya kutosha kupokea ugeni utakaowasili hapa ncbini.


“Tanzania kupitia serikali hii ya awamu ya tano imeridhia mashindano haya yafanyika hapa Tanzania na yanafanyika mwaka huu 2019.”


“Serikali imejiandaa kupokea wageni wote wanaokuja kushiriki mashindano yatakayofanyika nchi na serikali inaendelea na maandali hayo kwa kushawishi sekta zote zitakazonufaika na uwepo wa wageni hao.”


“Kupitia mashindano haya tum... Continue reading ->


Source: Shaffih DaudaRead More