WAZIRI MKUU APOKEA WATALII 330 KUTOKA CHINA - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI MKUU APOKEA WATALII 330 KUTOKA CHINA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewapokea watalii 330 wakiwemo wafanyabiashara na wawekezaji kutoka jimbo la Zhejiang, China ambao waliwasili jana usiku kwenye uwanja wa ndege wa KIA.
Watalii hao ni kundi la kwanza miongoni mwa watalii 10,000 ambao wanatarajiwa kutembelea Tanzania mwaka huu, chini ya mpango unaosimamiwa baina ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Bodi ya Utalii Tanzania na kampuni ya TouchRoad International Holding Group ya China.
Akizungumza na watalii hao kwenye chakula cha jioni kilichoandaliwa kwenye hoteli ya Mount Meru jana usiku (Jumapili, Mei 12, 2019), Waziri Mkuu alimshukuru Mwenyekiti wa Touchroad Group, Bw. Liehui He kwa kuwaunganisha Watanzania na Wachina kupitia mpango wake wa kukuza utalii.
“Mbali na kutuunganisha Watanzania na Wachina, tunakushukuru pia kwa kuamua kuitangaza Tanzania kuwa nchi yenye fursa nyingi za kitalii duniani,” alisema.
Waziri Mkuu alitaja vivutio vingine vilivyopo ambavyo watalii hao wanaweza kuvifurahia kuwa ni mbuga za Ngorongoro, Sere... Continue reading ->Source: KajunasonRead More