WAZIRI MKUU ASIKITISHWA WIZI KWENYE MRADI WA NSSF DEGE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI MKUU ASIKITISHWA WIZI KWENYE MRADI WA NSSF DEGE*Aagiza wakurugenzi wakuu wa NSSF, AZIMIO, Kamishna TRA wakutane.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea mradi wa nyumba unaojengwa kwa ubia kati Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kampuni ya Azimio Housing Estate Limited katika eneo la Dege Beach Kigamboni na kutamka kuwa amesikitishwa na uharibifu wa mali na wizi unaendelea kwenye eneo hilo.
Amewaagiza Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, William Erio na Mkurugenzi wa Mkuu kampuni ya Azimio Housing Estate Limited, Mohammed Iqbal wakutane na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere ili wajadiliane namna ya kudhibiti wizi na kuimarisha ulinzi. 
Waziri Mkuu alitembelea eneo la mradi huo jana jioni (Jumatatu, Novemba 12, 2018) ambapo baada ya kufika katika eneo ambalo linajengwa nyumba zaidi ya 7,000 alionesha kusikitishwa na uharibifu wa mali na wizi unaoendelea na kutoa maagizo kwa wahusika.
“Kuna mpango gani wa ulinzi wa mali hapa, mali zinaendelea kuibiwa, tutakuja kuanza ujenzi hapa na kukuta hakuna mali hata moj... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More