WAZIRI MKUU ATEMBELEA KIWANDA CHA PAMBA FRESHO SHINYANGA....ASEMA SERIKALI ITALINDA WANUNUZI WA PAMBA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI MKUU ATEMBELEA KIWANDA CHA PAMBA FRESHO SHINYANGA....ASEMA SERIKALI ITALINDA WANUNUZI WA PAMBA


Na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Kassim Majaliwa ametembelea kiwanda cha Kuchambua pamba cha Fresho kilichopo katika eneo la Ibadakuli Mjini Shinyanga na kujionea hali halisi ya ununuzi wa pamba kutoka kwa wakulima unaofanywa na Kampuni ya Fresho Investment Company Limited. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametembelea kiwanda cha Fresho kinachomilikiwa na Kampuni ya Fresho Investment Company Limited leo Ijumaa Agosti 9,2019 wakati akiwa kwenye ziara yake ya siku moja mkoani Shinyanga. 
Akizungumza kiwandani hapo,Waziri Mkuu aliwahakikishia wakulima wa pamba kuwa pamba yao itanunuliwa kwani lengo la serikali ni kuondoa pamba mikononi mwa wakulima. 
"Nipo kwenye ziara kwenye mikoa inayolima pamba lengo la kufuatilia mwenendo wa masoko ya pamba.Nikiwa hapa Shinyanga nimeshuhudia wingi wa pamba inayoletwa na wananchi kwenye masoko,kwetu sisi kama serikali ni jambo kubwa sana kiuchumi kwani pamba kwa Tanzania ni uchumi mkubwa,pamba imetupa hesh... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More