WAZIRI MKUU ATOA SIKU MBILI KWA AFISA ELIMU MULEBA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI MKUU ATOA SIKU MBILI KWA AFISA ELIMU MULEBA


* Ifikapo Jumatano awe amepeleka walimu shule ya msingi Rwenzige
*Ina wanafunzi 216 wa darasa la awali hadi la nne bila mwalimu

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa siku mbili kwa Kaimu Afisa Elimu (Msingi) wa wilaya ya Muleba, mkoani Kagera Bw. Bukuru Malembo awe amepeleka walimu wawili katika shule ya msingi iliyoko kwenye kitongoji cha Rwenzige kwa kuwa haina mwalimu hata mmoja.

Shule hiyo yenye madarasa wawili na ofisi moja ya mwalimu ina jumla wanafunzi 216 wa darasa la awali hadi la nne, ilijengwa na wananchi ambapo wanafunzi wake wanafundishwa na mwananchi mmoja aliyemua kujitolea ili kuwapunguzia watoto kutembea umbali wa kilomita 16 kwenda kusoma katika shule ya kijiji cha Kiteme.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana (Jumatatu, Oktoba 8, 2018) baada ya wanafunzi wa shule hiyo kuwasilisha malalamiko yao kwa njia ya bango wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kiwanja cha kituo cha afya Kimeya, baada ya kukagua majengo ya kituo hicho.

... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More