WAZIRI MKUU AWAPONGEZA PRECISION AIR - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI MKUU AWAPONGEZA PRECISION AIR

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewapa sifa Shirika la Ndege Precision Air kwa huduma nzuri wanazotoa kwa wananchi.
Hayo aliyasema baada ya kupita katika banda la shirika hilo wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Kimataifa ya Utalii Nchini yanayofanyika kwenye Ukumbi  wa Kimataifa wa JNICC.
Maonesho hayo yamezinduliwa leo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa yamehusisha makampuni na watoa huduma za utalii zaidi 300 duniani.
Akizungumza na Michuzi Blog, Meneja Masoko na Mahusiano wa Precisoon Air Hillary Mremi amesema kuwa wamefurahi sana kuweza kupewa pongezi na Waziri Mkuu baada ya kuona juhudi zao katika usafiri wa anga.
Mremi amesema kuwa wamekuwa wanatoa huduma ya usafiri wa anga kwa kipindi cha miaka 25 na wamefanikiwa kupeleka huduma hiyo sehemu tofauti katika nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Uganda na Kenya.
Mbali na hilo, Mremi amesema kuwa katika banda lao ndani ya maonesho ya kitalii wanatoa huduma ya ukataji tiketi kuelekea sehemu mbalimbali kwa punguzo la b... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More