WAZIRI MKUU AWATAKA VIONGOZI WA WILAYA YA KYERWA WAJIPIME - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI MKUU AWATAKA VIONGOZI WA WILAYA YA KYERWA WAJIPIME

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amechukizwa na biashara za magendo zinazoendelea katika wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera, hivyo amewataka viongozi wa wilaya hiyo wajipime wenyewe.  Pia, Waziri Mkuu amemuagiza Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Kagera Bw. Adam Ntogha kumsimamisha kazi Afisa wa Forodha katika mpaka wa Mulongo Bw. Peter Mtei kwa tuhuma za kujihusisha na biashara za magendo.  Ametoa agizo hilo Jumanne, Oktoba 9, 2018 wakati akizungumza na viongozi wa mkoa wa Kagera katika kikao cha majumuisho ya ziara yake ya kikazi ya siku nne mkoani hapa kilichofanyika mjini Bukoba.  “Biashara za magendo zinafanyika bila ya wao kuchukua hatua, mnatia aibu yaani hakuna kazi inayofanyika. Viongozi wa wilaya ya Kyerwa mjipime wenyewe, mialo mingi katika wilaya yenu inatumika kwa biashara ya magendo na butura.”  Waziri Mkuu aliongeza kuwa katika mwalo wa Mulongo ulipo kwenye eneo ambalo Tanzania inapakana na nchi za Uganda na Rwanda, biashara za magendo na butura zina... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More