Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ataka uhalifu udhibitiwe - Kwanza TV | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ataka uhalifu udhibitiwe

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Wakuu wa Polisi katika nchi za Mashariki mwa Afrika, waweke mikakati thabiti ya kukabiliana na magenge yote ya uhalifu unaovuka mipaka ili wahalifu hao wasipate mahali salama pa kufanya uhalifu bila mkono wa dola kuwafikia.


Pia, Waziri Mkuu amewataka viongozi hao wadumishe ushirikiano baina yao ili waimarishe utendaji bila kujali mipaka ya nchi zao kwa sababu wahalifu wanatumia sana udhaifu wa kukosekana  ushirikiano madhubuti miongoni mwa nchi hizo.


Waziri Mkuu ameyasema hayo leo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 21 wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi Mashariki mwa Afrika (EAPCCO), uliofanyika kwenye ukumbi wa AICC, jijini Arusha. Amefungua mkutano huo  kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli.


Amesema mfumo wa uhalifu duniani kwa sasa unachukua sura mpya kufuatia kukua kwa teknolojia hususani ya habari na mawasiliano, uhuru wa watu na bidhaa kuvuka mipaka pamoja na kuondolewa vikwazo vingi hususani visivyo vya kiforodha, hivyo kumewezesha kuwepo kwa ... Continue reading ->


Source: Kwanza TVRead More