WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASISISTIZA MAWAZIRI WA SADC KUSIMAMIA MAENDELEO YA TEKNOLOJIA - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASISISTIZA MAWAZIRI WA SADC KUSIMAMIA MAENDELEO YA TEKNOLOJIA

 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa wanakutana kwa siku mbili kuanzia leo Septemba 19-20, 2019 jijini Dar es Salaam. Picha zote na Matokeo Chanya+.
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka mawaziri wanaoshughulikia tehama, habari, uchukuzi na hali ya hewa kutoka nchi 16 wanachama wa Jumuiya ya maendeleo ya nchi kusini mwa Afrika (SADC) kusimamia maendeleo ya teknolojia.
Hayo ameyasema leo Septemba 19, 2019 wakati akizindua mkutano wa mawaziri hao, ambao ulitanguliwa na majadiliano yaliyowakutanisha makatibu wakuu na viongozi wa juu wanaoshughulikia sekta hizo kutoka nchi wanachama ambao walikaa kwa siku tatu kabla ya baraza la mawaziri lililoanza juzi.
Kati ya maagizo hayo ni pamoja na kushughulikia masuala ya mtandao, mkakati wa posta kuurejesha katika teknolojia ya sasa, kuondoa vikwazo vya kibiashara ... Continue reading ->


Source: KajunasonRead More