WAZIRI MKUU KUFUNGUA MKUTANO WA WAKUU WA VYOMBO VYA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA KANDA YA AFRIKA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI MKUU KUFUNGUA MKUTANO WA WAKUU WA VYOMBO VYA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA KANDA YA AFRIKA

Na Said Mwishehe,Globu ya jamiiWAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano wa 28 wa Wakuu wa vyombo vinavyopambana na dawa za kulevya Kanda ya Afrika.
Akizungumza Dar es Salaam leo Kamishna wa Uhuduma wa  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini Valite Mwashusa amesema mkutano huo utaanza Septemba 17 hadi Septemba 21 mwaka huu.
Amefafanua utafanyika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNICC) jijini Dar es Salaam na lengo ni kubadilisha uzoefu na kupanga mikakati ya pamoja kuhusu udhibiti na mapambano dhidi ya dawa za kulevya.
"Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na dawa za kulevya na vitendo vya uhalifu itaratibu mkutano huo," amesema Mwashusa.
Amesisitiza mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na sababu za mkutano kufanyika nchini imetokana na nchi hizo 54 kutambua jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano katika kupamb... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More