WAZIRI MKUU, MAJALIWA AMPONGEZA MWAKINYO KWA USHINDI WA UINGEREZA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI MKUU, MAJALIWA AMPONGEZA MWAKINYO KWA USHINDI WA UINGEREZA

Na Mwandishi Wetu, DODOMA
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa amempongeza bondia Hassan Mwakinyo kwa ushindi wake wa TKO dhidi ya Muingereza, Sam Eggington Uwanja wa Arena Birmingham, zamani Barclaycard Arena mjini Birmingham, England Jumamosi iliyopita.
Mwakinyo aliushitua ulimwengu baada ya kummaliza Eggington kwa TKO katika raundi ya pili kuelekea pambano kuu jana kati ya Muingereza, Amir Khan na Samuel Vargas Colombia anayeishi Canada. Khan alishinda kwa pointi za majaji wote.
“Na nimpongeze pia mwanamasumbiwi wa Kitanzania, Hassan Mwakinyo kwa kumchapa bondia Muingereza, Sam Eggington kwenye raundi ya pili ya pambano lao la masumbwi lililofanyika huko Birmingham nchini Unigereza,".
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia) amempongeza bondia Hassan Mwakinyo (kushoto) kwa ushindi wake wa TKO Uingereza 

"Hongereni sana wanamichezo wetu na endelezeni moyo huo wa kizalendo mliouonyesha katika kulitangaza taifa letu,”alisema Waziri Mkuu.
Baada ya maele... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More