Waziri Mkuu Majaliwa Atoa Ufafanuzi 'sintofahamu' ya wakulima bei ya korosho - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Waziri Mkuu Majaliwa Atoa Ufafanuzi 'sintofahamu' ya wakulima bei ya korosho


Waziri Mkuu Majaliwa Atoa Ufafanuzi 'sintofahamu' ya wakulima bei ya korosho

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa ufafanuzi kuhusu uamuzi wa kuwalipa wakulima Sh2,600 kwa kila kilo moja ya korosho badala ya Sh3,300 kama ambavyo Serikali ilitangaza wakati wa mchakato wa kuzinunua mwaka jana.

Majaliwa ametoa ufafanuzi huo leo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la papo kwa papo aliloulizwa na mbunge wa Liwale (CCM), Zubery  Kuchauka.

Katika swali lake, Kuchauka amesema wakulima walio wengi  bado hawajapata fedha zao wakati Serikali imeshachukua korosho zao huku baadhi wakilipwa kidogo na  wengine wakilipwa Sh2,600  badala ya Sh 3,300 kama ilivyotangazwa na Rais John Magufuli.

Katika maelezo yake, Majaliwa amesema tamko la Rais Magufuli kununua korosho kwa Sh3,300 kwa kilo moja linahusu korosho daraja la kwanza na bodi ya zao hilo  ina sheria inayoeleza madaraja yalivyo.

“Kuna sheria inayoeleza korosho za daraja la pili zitauzwa kwa bei ya asilimia 80 ya daraja la kwanza. Ile ya Sh2,600 ni mahesabu yamefanyika ya asilimia 80 ya bei ya korosho daraja la kw... Continue reading ->

Source: Mwanaharakati MzalendoRead More