WAZIRI MKUU MSTAAFU, MIZENGO PINDA ATOA NENO KWA ATCL - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI MKUU MSTAAFU, MIZENGO PINDA ATOA NENO KWA ATCL

 Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda amelishauri Shirika la ndege la Tanzania ( ATCL) kufanya kazi kwa pamoja na Bodi ya Taifa ya Utalii (TTB) kwa lengo la kuongeza idadi ya watalii wanaokuja nchini kwa shughuli za utalii.
Amesema TTB na ATCL wanategemeana sana katika utendaji wa kazi zao hivyo lazima wafanye kazi kama timu.
Amesema Taasisi hizo zikishirikiana kikamilifu zitachochea ukuaji wa uchumi kwa kuongeza idadi ya watalii wanaokuja nchini kwa kutumia ndege zetu.
"Kwa sasa tuna usafiri wa uhakika tofauti na mwanzo hivyo ni lazima tuone mabadiliko kwenye sekta ya utalii" alisema Mhe. Pinda.Amewakikishia kuwa endapo watafanya kazi kwa umoja wataweza kufikia malengo makubwa na kupelekea nchi kuwa na uchumi wa kati.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Ladsilaus Matindi amesema hadi hivi sasa wamekuwa na utaratibu wa kukutana na TTB mara mbili kwa wiki kwa lengo la kujadiliana na kupanga mikakati ya maendeleo baina yao.
Ameongeza kuwa hadi hivi sasa wameshapiga hatua kubwa kutokan... Continue reading ->


Source: KajunasonRead More