WAZIRI MPINA ATOA SIKU SABA KWA MAKATIBU WAKUU WA KILIMO NA MIFUGO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI MPINA ATOA SIKU SABA KWA MAKATIBU WAKUU WA KILIMO NA MIFUGO

Na John MapepeleWaziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ametoa siku saba kwa makatibu wakuu wa Kilimo na Mifugo kuwasilisha wizarani kwake taarifa ya kwanini bei ya mbegu za mahindi na mtama pamoja na gharama za uhimilishaji mifugo nchini ni kubwa licha ya uwepo wa usimamizi wa Serikali,pia kuendelea kuagiza mbegu za matunda na mbogamboga nje ya nchi ambazo zinaweza kuzalishwa hapa nchini.
Mbali na hilo, Waziri Mpina pia amezitaka Taasisi za TPRI,TFDA,TBS na Kurugenzi ya Huduma za Mifugo katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi kujitathmini upya utendaji kazi wao kama wanastahili kuwepo baada ya kushamiri kwa dawa na viuatilifu vya kilimo na mifugo feki na vilivyokwisha muda wa matumizi na kusababisha hasara kubwa kwa wakulima,wafugaji na Taifa kwa ujumla.
Akifungua maonesho ya Kilimo Nane Nane, Kanda ya Kaskazini yanayofanyika katika viwanja vya Themi jijini Arusha, Waziri Mpina alisema ni jambo la aibu kwa viongozi kuendelea kuwakutanisha wakulima na wafugaji katika maonesho hayo kila mwaka hu... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More