Waziri Mwakyembe ammwagia sifa Mwanamitindo Flaviana Matata - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Waziri Mwakyembe ammwagia sifa Mwanamitindo Flaviana Matata

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amempongeza Mwanamitindo wa Kimataifa, Flaviana Matata kwa juhudi za kusaidia watoto wa kike kupata elimu kwa kuwawezesha vifaa muhimu vya shule ikiwemo ada na madaftari.Akizungumza na waandishi wa habari leo, Jijini Dodoma Dkt. Mwakyembe amewataka vijana wa kitanzania kuiga mfano wa mwanamitindo huyo ili kuchangia katika ujenzi wa taifa.“Nawasihi vijana wengine wenye fursa kama za Flaviana Matata kuzitumia vizuri kwa kuhakikisha jamii inanufaika na mafanikio waliyoyapata” ameongeza Dkt. Mwakyembe.


Aidha, aliongeza kwa kueleza kuwa, Mwanamitindo huyo amekuwa ni Balozi mzuri katika kupeperusha bendera ya Taifa katika nchi mbalimbali za Ulaya.


Kwa upande wake Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza amempongeza Bibi. Flaviana kwa kuwa mfano bora kwa watoto wa kike kwa jinsi ambavyo amekuwa akisaidia watoto wa kike nchini.


Naye Mwanamitindo,Flaviana ameleza kuwa mbali na kujis... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More