WAZIRI MWIGULU ASEMA KWA SIMBA ILIPOFIKA ANAIPA BARAKA ZA USHINDI FAINALI YA SPORT PESA ILA... - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI MWIGULU ASEMA KWA SIMBA ILIPOFIKA ANAIPA BARAKA ZA USHINDI FAINALI YA SPORT PESA ILA...

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk.Mwigulu amesema kwa sasa anachoweza kukielezea kwa timu ya Simba anamuomba Mungu aifanikishe timu hiyo kuhsinda mchezo wa fainali wa michuano ya Sport pesa dhidi ya timu ya Gor Mahia ya nchini Kenya.

Simba ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu wametinga fainali ya michuano hiyo na kesho Jumapili watacheza mchezo wa fainali ya michuano hiyo na timu ya Gor Mahia ya Kenya.

Akizungumza na Michuzi Blog jijini Dar es Saalam jana Dk.Mwigulu amesema amefurahi Simba kuingia fainali na sasa anatoa baraka ili ishinde kombe la michuano hiyo.

Michuzi Blog baada ya kukutana na Waziri Mwigulu pamoja na mambo mengine ilitaka kufahamu nini kauli yake kwa Simba inayosubiri kucheza fainali hiyo."Kwangu niseme tu naipa baraka zote timu ya Simba ili ishinde kombe la michuano hiyo.Hiki ndicho nachoweza kukielezea kwa sasa.

"Mashabiki wa soka nchini Kenya baada ya mwaka jana moja ya timu yao kuchukua kikombe hicho walit... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More