WAZIRI MWINYI AKAGUA MIRADI YA BUNGE INAYOTEKELEZWA NA SUMA JKT - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI MWINYI AKAGUA MIRADI YA BUNGE INAYOTEKELEZWA NA SUMA JKT

Waziri wa ulinzi na jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Hussein Mwinyi ameridhishwa na hatua za utekelezaji wa miradi mitatu ya ujenzi wa Ofisi ya Bunge inayotekelezwa na Shirika la Uzalishaji la Jeshi hilo (SUMA JKT).
Mhe. Mwinyi alitoa pongezi hizo wakati alipotembelea Ofisi ya Bunge kwa ajili ya kukagua miradi hiyo akiwa ameambatana na Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Martin Busungu na Mkurugenzi Mtendaji wa SUMA JKT, Kanali Rajab Mabele.
“Nimeridhishwa hatua ya utekelezaji wa miradi mitatu inayotekelezwa na SUMA JKT ya ujenzi na ukarabati wa Ofisi ya Bunge, naishukuru Ofisi ya Bunge kwa kuliamini shirika la SUMA kwa ajili ya kutelekeza miradi hii,” alisema.
Kwa upande wake Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai  alilipongeza SUMA JKT kwa kuendelea kutelekeza miradi hiyo kwa ufanisi na kwamba hadi sasa miradi yote inaendelea vizuri.
Alitaja miradi hiyo kuwa ni Mradi wa Ujenzi wa Ofisi ya Bunge, ukarabati wa Jengo la Ofisi ya Bunge pamoja na ujenzi wa lift na ujenzi wa nyumba ya Katibu wa Bunge... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More