Waziri Ndalichako Azindua Baraza La Uongozi La NACTE - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Waziri Ndalichako Azindua Baraza La Uongozi La NACTE


Na Regina MkondeWAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako  leo tarehe 9 Agosti, 2018 amelizindua Baraza jipya la Uongozi la Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika jana tarehe 9 Agosti, 2018 katika ukumbi wa mikutano wa NACTE ulioko jijini Dar es Salaam, Prof. Ndalichako alilipongeza baraza lililomaliza muda wake, na kutoa maagizo kwa baraza jipya.
Prof. Ndalichako amelitaka baraza hilo kuendelea kusimamia pamoja na kudhibiti ubora wa elimu inayotolewa na vyuo hapa nchini.
Vile vile, Prof. Ndalichako amelitaka baraza hilo kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika vyuo vilivyosajiliwa na vitakavyosajiliwa hapa nchini, ili kuhakikisha elimu inayotolewa kwa wahitimu inakidhi soko la ajira.
Katika hatua nyingine, Prof. Ndalichako amelitaka baraza jipya la NACTE kuongeza juhudi katika kufanya utafiti wa soko la ajira ili liweze kuwashauri wawekezaji wanaotaka kuanzisha vyuo, kutoa mafunzo yanayokidhi soko la ajira.
H... Continue reading ->


Source: Mwanaharakati MzalendoRead More