WAZIRI NDALICHAKO: SERIKALI YA AWAMU YA TANO INAENZI YALE YOTE ALIYOISHI MWALIMU NYERERE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI NDALICHAKO: SERIKALI YA AWAMU YA TANO INAENZI YALE YOTE ALIYOISHI MWALIMU NYERERE


Na Humphrey Shao, Globu ya JamiiWaziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako amesema falsafa za Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere zimepata msukumo wa hali ya juu katika serikali ya awamu ya tano kwa kuwataka watanzania kufanya kazi kwa bidii.
Prof Ndalichako amesema hayo leo Mapema Jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua kongamano la Siku mbili katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kampasi ya Kivukoni  lililokuwa na Mada inayosema  'Falsafa ya Mwalimi Nyerere Juu ya Taifa la Kujitegemea na Maendeleo ya Viwanda'
"Mwalimu Nyerere alisisitiza kufanya kazi kwa bidii na udalifu na kusimamia msingi wa uzalendo kwani Serikali ya awamu ya tano chini Rais Dk. John Magufuli ameweza kusimamia neno la hapa kazi tu ambalo ni moja ya Falsafa ya Mwalimu Nyerere iliyosema kuwa kufanya kazi kwa bidii , Kazi ni Uhai na Kazi ni Utu hivyo tunapaswa kujiuliza hii falsafa ina umuhimu gani katika kufanikisha kuelekea nchi ya uchumi wa Viwanda"
Prof Ndalichako amesema kuwa kuna mam... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More