WAZIRI PROFESA NDALICHAKO AAGIZA VYUO VINAVYOTOA ELIMU YA 'UBABASHAJI' VIFUTWE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI PROFESA NDALICHAKO AAGIZA VYUO VINAVYOTOA ELIMU YA 'UBABASHAJI' VIFUTWE

 Na Said Mwishehe, Globu ya jamii 
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako ametoa maagizo kwa Baraza la Elimu ya Ufundi(Nacte)kutosita kuchukua hatua ikiwamo ya kuvifuta vyuo ambavyo vitabainika kutoa elimu kwa ubabaishaji.
Pia amelishauri Baraza hilo kuhakikisha linasimamia na kutoa muongozo kuhusu program mbalimbali za utoaji elimu ya ufundi ambayo ametaka iwe inaendana na soko la ajira nchini ili kuhakikisha Watanzania wanapata fursa ya kuajiriwa kwa ajili ya kufanya kazi katika miradi mikubwa inayoendelea nchini.
Profesa Ndalichako ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anazindua rasmi Baraza la Uongozi la Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi nchini ambalo Mwenyekiti wake ni Profesa John Kandoro.
Kuhusu vyuo ambavyo vinashindwa kutoa elimu bora, Profesa Ndalichako amesema baraza hilo lisisite kuchukua hatua ikiwamo ya kuvifutia usajili vyuo ambavyo vitabainika kushindwa kukidhi vigezo vilivyowekwa.
Amefafanua haiwezekani vijana wawe wanalipa fedha kwenye ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More