WAZIRI TIZEBA AAGIZA MAKAMPUNI YA MBEGU KUWEKA BEI ELEKEZI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI TIZEBA AAGIZA MAKAMPUNI YA MBEGU KUWEKA BEI ELEKEZI

Na Wankyo Gati, Arusha
Waziri wa kilimo, Charles Tizeba ameagiza wadau wa pembejeo nchini kuhakikisha wanaweka bei elekezi  ya mbegu katika vifungashio vya mbegu hizo ili kuwawezesha wakulima wasilanguliwe. Hayo ameyasema leo  wakati akifungua mkutano wa wadau wa mbegu uliolenga kupashana taarifa kuhusu maendeleo ya sekta ya mbegu katika kuhakikisha wanazalisha mbegu nyingi na zenye ubora hapa nchini. 
 Waziri Tizeba alisema kuwa , ni lazima vifungashio vyote vya mbegu viwekwe bei elekezi ili kuzuia watu wanaofanya ulanguzi na kusababisha wananchi kushindwa kununua kutokana na bei kubwa wanayotajiwa.
 "naombeni Sana kila kifungashio kitakachokuwa kimebeba mbegu kiwe na bei elekezi na naagiza kuundwa kwa kamati ya pamoja ya kufuatilia mfumo wa uzalishaji na hizo bei elekezi kwenye vifungashio vyote. "alisema Tizeba.
 Aidha Tizeba pia aliyataka makampuni ya mbegu yanayozalisha mbegu  nje ya nchi na kuuza hapa nchini kuzalisha mbegu hizo hapa hapa nchini ili kuongeza ajira na kuwezesha k... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More