WAZIRI UMMY AKABIDHI MADAWATI 40 SHULE YA SEKONDARI CHUMBAGENI JIJINI TANGA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI UMMY AKABIDHI MADAWATI 40 SHULE YA SEKONDARI CHUMBAGENI JIJINI TANGA

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto na Wazee Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) leo amekabidhia madawati 40 na viti katika shule ya sekondari ya Chumbageni Jijini Tanga ikiwa ni mpango wake wa kuhakikisha changamoto zilizopo kwenye sekta ya elimu zinapatiwa ufumbuzi. 
Halfa hiyo ya makabidhiano ilifanyika leo shuleni hapo na kuhudhuriwa na walimu, wanafunzi na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ,Diwani wa Kata ya Chumbageni Saida Gadafi wakiwemo viongozi wengine. Hatua ya kukabidhiwa madawati hayo shule ya Sekondari ya Chumnageni ilitokana na ombi la Diwani wa Kata ya Chumbageni Saida Gadafi ambaye alimueleza waziri Ummy uwepo wa uhaba wa madawati kwenye shule hiyo. 
Akizungumza namna alivyoweza kuipatia ufumbuzi changamoto hiyo, Waziri Ummy alisema baada ya ombi hilo aliwapata wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambao walilikubali na kumpatia kiasi cha sh, milioni 5.4 ambazo wameweza kununua madawa... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More