WAZIRI UMMY AKABIDHI MADAWATI 40 SHULE YA SEKONDARI CHUMBAGENI JIJINI TANGA - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI UMMY AKABIDHI MADAWATI 40 SHULE YA SEKONDARI CHUMBAGENI JIJINI TANGA

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto na Wazee Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) kulia akimkabidhi madawati 40 Diwani wa Kata ya Chumbageni (CC) Saida Gadafi kwa ajili ya shule ya Sekondari Chumbageni ili kuweza kukabiliana na upungufu uliopo kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Chumbageni Gabriel Habash. WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto na Wazee Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) kulia akiwa amekaa kwenye mmoja ya madawati 40 aliyoyakabidhi leo kwa shule ya Sekondari Chumbageni kushoto ni Diwani wa Kata ya Chumbageni (CC) Saida Gadafi ambaye alimuomba Waziri huyo madawati hayoi kwa ajili ya shule ya Sekondari Chumbageni ili kuweza kukabiliana na upungufu uliopo. WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto na Wazee Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) kushoto akifurahia jambo na wanafunzi wa shule ya Sekondari Chumbageni mara baada ya kuwakabidhi madawati hayo. WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto na Wazee Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) akizungumza wakati wa halfa hiyo kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Chumbageni Gabriel Habash na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya TangaThobias Mwilapwa.Diwani wa Kata ya Chumbageni (CC) Saida Gadafi akizungumza katika halfa hiyo ambapo alimshukuru Waziri Ummy kwa kuwapa msaada huo.Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Chumbageni Gabriel Habash akizungumza katika halfa hiyo ambapo alimshukuru Waziri Ummy kwa kuisaidia shule hiyo.Mwalimu Mkuu wa wa shule ya Sekondari Chumbageni Kavumo Juma Mziray akitoa hotuba yake. Sehemu ya wanafunzi wa shule hiyo wakifutiliana makabidhiano hayo. Sehemu ya madawati na viti ambayo yamekabidhiwa leo na Waziri Ummy kwa shule ya Sekondari Chumbageni.WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto na Wazee Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na waalimu wa shule ya Sekondari Chumbageni mara baada ya kukabidhi madawati hayo leo
NA MWANDISHI WETU, TANGA.
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto na Wazee Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) leo amekabidhia madawati 40 na viti katika shule ya sekondari ya Chumbageni Jijini Tanga ikiwa ni mpango wake wa kuhakikisha changamoto zilizopo kwenye sekta ya elimu zinapatiwa ufumbuzi.
Halfa hiyo ya makabidhiano ilifanyika leo
shuleni hapo na kuhudhuriwa na walimu, wanafunzi na viongozi mbalimbali
akiwemo Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ,Diwani wa Kata ya
Chumbageni Saida Gadafi wakiwemo viongozi wengine.Hatua ya
kukabidhiwa madawati hayo shule ya Sekondari ya Chumnageni ilitokana na
ombi la Diwani wa Kata ya Chumbageni Saida Gadafi ambaye alimueleza
waziri Ummy uwepo wa uhaba wa madawati kwenye shule hiyo.Akizungumza
namna alivyoweza kuipatia ufumbuzi changamoto hiyo, Waziri Ummy alisema
baada ya ombi hilo aliwapata wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya
Jamii (NSSF) ambao walilikubali na kumpatia kiasi cha sh, milioni 5.4
ambazo wameweza kununua madawati 40 na viti“Mh Saida umetenda
wajibu wako ipasavyo maana taarifa ya mkuu wa shule inasema kuna uhaba
wa viti 163ubawa wa meza 100 hivyo kupatina kwa hivyo vilivyokabidhiwa
leo kumepunguza nusu lakini nitaendelea kushirikiana nanyi “Alisema


“Kazi
nzuri inafanywa kwenye shule ya sekondari Chumbageni na nimeambiwa
kiwango cha ufaulu kinaongezeka mwaka hadi mwaka asilimia 51 hadi
asilimia 77 lakini pia nitoe pongeze kwa Halmashauri ya Jiji la Tanga
kutatua changamoto ya elimu sio watu kusubiri mpaka serikali kuu kwani
wamekuwa wakijiongeza na diwani Saida kutatua changamoto ya elimu kwenye
kata yake “Alisema.Hata hivyo alisema ataendelea kushirikiana
na madiwani kuhangaika ili aweze kupata fedha za ujenzi wa ofisi ya
walimu kwen ye shule hiyo lakini pia wanafunzi nitawaletea vitabu huku
akitoa wito kwa wananchi kushirikiana kuona namna ya kutatua changamoto
ya elimu sio kusubiri serikali pekee bali ni watu wote.“Nimshukuru
Rais kuanzisha sera ya elimu bure ambayo imewasaidia, watu wengi
...watu walikuwa wanaponda shule za kata wakati mimi nilipokuwa nasoma
shule zikuwa chache kutokana na kukosekana nafasi lakini leo hii zipo za
kutosha hivyo kuwasaidia watoto wa kike kuepushwa na ndoa za utotoni na
wavulana kuvuta bangi.Alisema leo hii Serikali chini ya Rais
Dkt John Magufuli imekuwa ilileta milioni 161 kila mwezi kwa Halmashauri
ya Jiji la Tanga kwa ajili ya elimu bure hii imesaidia sana lakini
wengine walikuwa wanakosa kwa sababu ya ada lakini tatizo la ada
limetatuliwa .Copyright 2007-2017 @KAJUNASON BLOG


Source: KajunasonRead More