WAZIRI WA AFYA AWATAKA WAGANGA WAKUU KUSIMAMIA MATUMIZI YA MAGARI YA KUBEBEA WAGONJWA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI WA AFYA AWATAKA WAGANGA WAKUU KUSIMAMIA MATUMIZI YA MAGARI YA KUBEBEA WAGONJWA

Na Stella Kalinga, SimiyuWaziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu amepiga marufuku magari ya kubeba wagonjwa (Ambulance ) kubeba watu au kitu chochote tofauti na wagonjwa na akawaagiza Waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya kote nchini,  kusimamia matumizi ya magari hayo na kuhakikisha yanatumika kwa matumizi yaliyokusudiwa kwa mujibu wa mwongozo.
Waziri Ummy ametoa agizo hilo Julai 12, 2018 katika uzinduzi wa Mradi wa TUWATUMIE wenye lengo la kuunganisha jamii hasa zile zilizo mbali na vituo vya tiba, ambao umezinduliwa katika Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, kuunganisha jamii zinazoishi maeneo magumu kufikiwa  na mfumo wa Huduma za Afya ambao umelenga kupunguza vifo  vya mama na Mtoto mkoani SIMIYU.
“Nimesikitishwa sana na kitendo cha gari la kubebea wagonjwa la Halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara kubeba dawa za kulevya, ninakemea jambo hili kwa nguvu zangu zote na ninawataka waganga wakuu wa mikoa na wilaya kote nchini kusimamia matumizi ya ma... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More